CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR
(SUZA)
SKULI YA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIGENI
(SKILUKI)
IDARA YA KISWAHILI
JINA LA KOZI: NADHARIA YA FONETIKI NA
FONOLOJIA YA KISWAHILI
KODI YA KOZI: LK 2101
MHADHIRI: MR. AMOUR A. KHAMIS
MWAKA: MWAKA WA PILI
MUHULA: MUHULA WA KWANZA
KAZI: KAZI YA
NYUMBANI
WASHIRIKI: ABDI NASSOR
HAJI BAE/17/18/125/TZ
MWANAIDI
BILAL KASIM BAE/17/18/132/TZ
SUALI: ‟
Linganisha na tofautisha dhana ya fonetiki iliyotolewa na Khamis na Masamba”
TAREHE YA
KUWASILISHA: 20/11/2019
Kwa mujibu wa Khamis
(2011) "Fonetiki ni tawi la lughawiya fafanuzi linalochunguza taaluma ya
uchambuzi na uchanganuzi wa vitamkwa vya lugha mbalimbali zitumiwazo na
mwanaadamu katika hali ya utamkwaji, usafirishwaji na usikiwaji pamoja na
uandikwaji wa vitamkwa hivyo kifonetiki kutoka uandikwaji wa kiothografia ".
Vilevile Masamba, (2007) kaeleza
maana ya fonetiki kuwa “ni tawi ambalo
linajisughulisha na uchunguzi na uchanganuzi wa taratibu zote zonazohusiana na
utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binaadamu
kwa ujumla”
Hivyo basi, kutokana na fasili
zilitolewa na wataalamu hao hapo juu kwa
ujumla wake tunapata maana kuwa fonetiki ni tawi la lughawiya ambalo
dhumuni lake ni kuchunguza na kuchambua
jinsi vitamkwa au sauti za lugha mbali mbali zinavyotamkwa, kusafirishwa ( kupitia
mkondo hewa ) na jinsi zinavyosikika.
Katika kuangalia vitamkwa au sauti za lugha, tunaangalia kupitia matawi ya
fonetiki ambayo ni fonetiki matamshi,
fonetiki akustika na fonetiki masikizi.
Maana hizo hapo juu zinaelekea kulingana
kwa ujumla wake pia kutofautiana kwa baadhi ya vipengele kama ifuatavyo:
Kwa upande wa kufanana au
kulingana wataalamu hao wamefanana katika kuzungumzia swala la sauti za lugha
ya mwanaadamu. Fonetiki hushughulikia sauti za lugha pekee na si sauti
nyenginezo zinazotokana na binadamu kama vile kucheka, kulia au hata chafya
ambapo sauti hizi haziwezi kuwa ni vitamkwa vya lugha. Hivyo wataalamu hawa
walipotoa fasili ya fonetiki
wamezingatia suala la msingi ambalo ni sauti za lugha au vitamkwa vya lugha ya
mwanaadamu ambavyi kimsingi ndivyo vyenye kushughulikiwa na tawi hili. Wanafonetiki
huchunguza jinsi sauti za lugha zinavotamkwa, kusafirishwa Kati ya kimyaa cha
msemaji na sikio la msikilizaji na jinsi zinavyofasiriwa katika ubongo wa
msikilizaji.
Vilevile, wataalamu wote wawili
wamezungumzia tawi la lughawiya. Kimsingi hasa fonetiki ni tawi la lughawiya:
ambapo tawi hili hujikit akatiak uchanganuzi wa ndani kabisa wa vitamkwa vya
lugha za binnadamu. Katika maana za wataalamu wa hapo juu tunaona kuwa
wataalamu hao hawakuacha kuingiza maneno hayo ambayo ni tawi la lughawiya au tawi la
isimu, hivyo huwezi kuipata fonetiki kwenye fani yoyote isipokua katika
isimu au lughawiya.
Pia, wataalamu wote wametumia neno
mwanaadamu. Mwanaadamu ndie kiumbe pekee ambae ana uwezo wa kuzalisha vitamkwa
vya lugha ambavyo vinaweza kusikika, kufahamika na kuandikika na pia binadamu
pekee ndie mwenye uwezo wa kutumia lugha. Hivyo, wataalamu hawa hawakuacha kulitumia
neno hili kwani wanyama hutoa milio tu ambayo inasikika ila haiwezi kufahamika
wala kuandikika wala kubainishwa kifonetiki bali ni njia yao ya mawasiliano.
Kwa kuongezea, wataalamu hawa
wamezungumzia suala la utamkwaji, usafirishwaji na usikiwaji wa
sauti za lugha. Hii ina maana kua Khamis na Massamba wanakubaliana kuwa sauti
zote za lugha lazima zitamkike (kutoka katika kinywa cha binaadamu),
zisafirishwe ( sauti ziwe ni zenye kubebwa na mkondo hewa ) na kusikika (
msikilizaji awe anazisikia na kuzifahamu ). Katika kutoa fasili zao
wamezingatia matawi ya fonetiki ambayo ni fonetiki matamshi (utamkwaji ), fonetiki akustika (usafirishwaji) na fonetiki masikizi (usikiwaji)
Kwa upande mwengine, Khamis na
Massamba katika fasili yao ya fonetiki wametofautiana kwenye vipengele
vichache kama ifuatavyo:
Massamba kwenye fasili ya dhana
fonetiki kaeleza kuwa fonetiki ni taaluma inayojihusisha na utoaji wa sauti
za lugha….ikiwa na maana kua
fonetiki inahusiana kule tu sauti za lugha kutolewa katika kinywa cha msemaji.
Ambapo Khamis kaelezea kua fonetiki inahusiana na uchambuzi na
uchanganuzi wa vitamkwa vya lugha ikiwa na maana kuwa Khamis yeye
kazingatia uchambuzi na uchanganuzi wa sauti hizo ambazo huzalishwa kutoka
katika kinywa cha msemaji.
Kwa ujumla wake licha ya toafati
ndogo ndogo zilizojitokeza kwenye fasili za wataalamu hao ila kwa kiasi flani
wameweka wazi lile lengo hasa na kazi hasa ya fonetiki kua ni kuchunguza sauti
za lugha na si vyenginevyo. Utoafauti huo uliotokea ni kile kinachoitwa upekee
wa mtu, hii ni kwa sababu mada moja haiwezi kulezewa sawa sawa na watu wawili
tofauti, kila mmoja ataelezea kiupande wake ila lengo na dhumuni huwa ni
lilelile.
MAREJEO
Khamis,A. (2011). Uchambuzi wa Kiswahili Fasaha: Sarufi na
Lughawiya. Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani. Zanzibar.
Massamba, D. (2007).Fonolojia ya Kiswahili Sanifu.Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili. Dar Es Salaam.
Mgullu, S.R. (1999). Mtaala wa Isimu:Fonetiki , Fonolojia na
Mofolojia ya Kkiswahili. Nairobi, Printwell Industries.
No comments:
Post a Comment
Thanks